Kiwembe Lyrics
Kiwembe Song Lyrics
Hata uwe na pesa
Ujaze benki kuu
Ipo siku utajionea
Hayana maana
Yatakupa presha
Ukae roho juu
Hata uwe bilionea
Faida hayana
Unajua mapenzi ni siri
Aloyaleta ni nani
Yamewashinda walimu
Yamevuruga wengi wenye akili
Na manguri darasani
Na vyeti vya kuhitimu
Hodari wa mapenzi nani mnitajie
Anyoshe kidole tumuone
Maua yake tumwagie
Hodari wa mapenzi nani mnitajie
Apite mbele tumuone
Au wote wenzangu na mie
Penzi kiwembe (Kiwembe)
Mapenzi kiwembe
Yameuchanachana moyo
Mapenzi kiwembe
Mapenzi kiwembe (Kiwembe)
Mapenzi kiwembe
Yameuchanachana moyo
Mapenzi kiwembe
Hayachagui dini, kabila
Gwiji wa imani
Uwe padri ama shekhe
Utakesha msikitini ila bila
Ulale kanisani
Na miti shamba uoge
Unaweza kuwa una mpenzi
Ukadhani mpenzi
Kumbe ana mpenzi wake
Akakufanyia ushenzi
Atie dosari penzi
Akimaliza shida zake
Unajua mapenzi ni siri
Aloyaleta ni nani
Yamewashinda walimu
Yamevuruga wengi wenye akili
Na manguri darasani
Na vyeti vya kuhitimu
Hodari wa mapenzi nani mnitajie
Anyoshe kidole tumuone
Maua yake tumwagie
Hodari wa mapenzi nani mnitajie
Apite mbele tumuone
Au wote wenzangu na mie
Penzi kiwembe (Kiwembe)
Mapenzi kiwembe
Yameuchanachana moyo
Mapenzi kiwembe
Mapenzi kiwembe (Kiwembe)
Mapenzi kiwembe
Yameuchanachana moyo
Mapenzi kiwembe
Community Thoughts .
0 CommentsLeave a Reply
Your email address will not be published. Required fields are marked *
No comments yet
Be the first to share your thoughts about these lyrics!